Mechi za makundi ya kufuzu
kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi zinafikia ukikongoni
huku ikishuhudiwa nchi kadhaa zikifuzu na nyingine maarufu zikikosa
nafasi ya kufuzu ambapo nchi kama Marekani na Uholanzi zikikosa sifa ya
kucheza fainali hizo.
Wakati Marekani, Chile na
Uholanzi zikikosa Fainali za Kombe la Dunia 2018, tayari timu 22 tayari
zimejihakikishia kucheza ikiwa ni pamoja na mwenyeji Urusi katika
fainali hizo zitakazoshirikisha timu 32.
Zilizofuzu moja kwa moja kutoka katika hatua ya makundi ni;
Bingwa mara tano Brazil, mabingwa watetezi Ujerumani, pamoja na Argentina,
Ubelgiji, Colombia, Costa Rica, England, Misri, Ufaransa, Iceland,
Iran, Japan, Mexico, Nigeria, Panama, Poland, Ureno, Saudi Arabia,
Serbia, Korea Kusini, Uhispania na Uruguay.Timu nane kutoka Bara la Ulaya zitacheza mechi za mtoano ili kupata timu nne zitakazokamilisha idadi ya timu 14 za Ulaya kufuzu fainali hizo ambapo hadi sasa Bara hilo lina timu 10 ambapo ratiba ya mechi hizo itatolewa October 16 mjini Zurich huku michezo hiyo ikitarajiwa kuchezwa November 9 hadi 11 kwa michezo ya awali na marudiano itakuwa November 12 hadi 14.
Switzerland, Italy, Denmark, Croatia, Ireland Kaskazini, Jamhuri ya Ireland, Sweden na Ugiriki.
Kwa upande wa Amerika ya Kusini, tayari timu nne zimeshafuzu lakini kuna nafasi moja ambapo Peru iliyomaliza nafasi ya tano itacheza mechi ya mtaono dhidi ya New Zealand.
Amerika ya Kaskazini inazo nafasi tatu kujumlisha nafasi ya mtoano ambapo hadi sasa zilizofuzu moja kwa moja ni Mexico, Costa Rica na Panama huku Honduras ikicheza na Australia kwenye mtoano kupata nafasi ya nne.
Afrika inazo nafasi tano kwenye fainali hizo ambapo hadi sasa ni nchi mbili zilizofuzu ambazo ni Nigeria na Misri huku bado michezo ya makundi ikiendelea.
0 comments:
Post a Comment