TAYARI KIJAZI AKABIDHIWA KIJITI CHA SEFUE


Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, amemwapisha Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Jijini Dar es Salaam jana.

Rais Magufuli amemteua Balozi Mhandisi Kijazi kushika nafasi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Balozi Ombeni Sefue, ambaye amesema atampangia kazi nyingine.

Kabla ya uteuzi huo, Balozi Mhandisi Kijazi alikuwa mwakilishi wa Tanzania nchini India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal mwenye makazi yake jijini New Delhi, India kuanzia mwaka 2007 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi.

0 comments:

Post a Comment