Mgombea urais Donald Trump akutana na mgombea mwenzake

Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani Ben Carson, amekutana  Mgombea urais  Donald Trump na
kutangaza rasmi kumuunga mkono Bilionea huyo anayetikisa katika  kampeni za uchaguzi wa awali nchini Marekani.
Kulingana na vyombo vya habari vya Marekani, Carson ambaye alitangaza wiki iliyopita kuachana na azma yake ya kugombea Urais, amekutana na Trump na kutangazakumuunga mkono Bilionea huyo katika mkutano na waandihi wa habari utakaofanyika katika jimbo la Florida.
Wakati huo huo Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Marco Rubio amemshtumu  vikali Donald Trump kwa kusema kuwa Uislamu unachukia Marekani .
Licha ya wagombea kutangaza sera zao nyingine kwa amani lakini mjadala wa swala la Uislamu, kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Trump na wagombea wengine huku wenzake wote wakitofautiana kutokana na kauli zake zinazoonekana kama zenye msimambo mkali.

0 comments:

Post a Comment