Ndoa ya Mwanamuziki Young D na Mrembo Tunda Inanukia...Wazazi Wameshaafikiana

Mbongo-Fleva, David Genzi ‘Young D’ na mwandani wake ambaye ni muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Tunda Sebastian, wameibua gumzo kwa taarifa kuwa wapo kwenye mikakati mizito ya kufunga pingu za maisha kutokana na upendo wa kweli walionao na jinsi wanavyoendana bila kujali udogo wao kiumri.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichopo karibu na Tunda, eti ndoa ya wawili hao kwa sasa inanukia kwani ishu hiyo hata wazazi wa pande zote mbili wameshaikubali na kilichobaki ni siku ya cherekochereko tu japokuwa watu hawaamini kama hilo linawezekana.

Baada ya kuunyaka ‘ubuyu’ huo, paparazi wetu alianza kwa kumvutia waya Young D ambaye simu yake haikuwa hewani lakini kwa upande wake Tunda alipotafutwa aliangua kicheko na kusema kuwa, siku zote watu wenye mapenzi ya kweli lazima wawe na malengo ya kuoana.

“Hakuna mwenye pingamizi kati yetu kuhusu hilo tunapendana na tunaendana ndiyo maana tukaanika uhusiano wetu, kwani tumeshatambulishana kwa wazazi, kwao najulikana na kwetu pia wanamjua, wapenzi wanaopendana kweli kifuatacho huwa ni ndoa tu,” alisema Tunda.

0 comments:

Post a Comment