EDWARD Lowassa: Rais Magufuli ni Mfano wa Viongozi wa Afrika Wasio na Maono

Edward Lowassa leo ameamua kumuelezea ukweli rais Magufuli kuwa ni miongoni mwa marais wa Afrika wasio na maono. Lowassa pia amesema kuwa Tanzania chini ya Magufuli itakosa kabisa ubunifu.

Hayo yanajiri baada ya rais John Magufuli kuzuia mambo mengi kwa lengo la kubana matumizi. Huku wataalam mbalimbali wakikwama kuwekeza kwenye taaluma baada ya kuzuiwa kupata mafunzo mbalimbali nje na ndani ya nchi.

Aidha rais Magufuli amekuwa akitoa hotuba kwa hisia kali hali inayowafanya wasaidizi wake kuingiwa na woga kwenye uthubutu.

"Magufuli ewafanya wasaidizi wake kukosa kabisa ubunifu na uthubutu wa kufanya maamuzi. Tanzania chini yake haitakuwa na jipya" amesema Lowassa.

Aidha Lowassa amesema kuwa sera ya elimu bure kwa Magufuli imekuwa "zero" baada ya kuiga.

0 comments:

Post a Comment