Mashimo Yaliyouwa Watano Geita Yafungwa, Ili kufanya uchunguzi wa kina wa chanzo cha ajali

Serikali imeyafunga mashimo yote yanayodaiwa kuwa na dhahabu katika kata ya Mgusu Mkoani Geita baada ya watu watano kufariki dunia kwa kufukiwa na kifusi, ili kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha kushuka kwa kifusi hicho.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Medard Kalemani ametoa tamko la kufunga mashimo hayo mara baada ya kutembelea eneo hilo na kuwapa pole ndugu na jamaa walioondokewa na wapendwa wao.

Amesisitiza Serikali imeamua kuchukua uamuzi huo wa haraka, ili kufanya uchunguzi wa kina na kutafuta vifaa vya kuboresha eneo hilo kwa kuwa linamilikiwa kisheria na wachimbaji wana SACCOS ya Mgusu.

Baadhi ya wachimbaji wanaofanya shughuli zao katika maeneo hayo walikuwa na haya ya kusema kuhusu ufungwaji wa eneo hilo kwa muda.

March 9 majira ya saa tisa mchana watu wanane waliokuwa wakichimba mawe yadhaniwayo kuwa na dhahabu katika machimbo ya Mgusu walifukiwa na kifusi ambapo watu watano walipoteza maisha akiwemo mwanamke mmoja.

0 comments:

Post a Comment