Kinyang’anyiro cha Urais Marekani, KINYANG’ANYIRO CHA URAIS MAREKANI

Mgombea wa nafasi ya urais wa Marekamni kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump amesitisha mkutano wake uliokuwa ufanyike katika ukumbi wa midahalo wa chuo kikuu cha Illinois,Cincinati akidai hali ya usalama haikuwa nzuri na watu wengeweza kuumia.

Hata hivyo jeshi la polisi kupitia msemaji wake katika mji huo limesema jeshi hilo lilikuwa limejipanga vyema kukabiliana na matukio yoyote ya uvunjifu wa amani hivyo isingeweza kutokea jambo lolote la kuhatarisha amani katika mkutano huo.

Mashabiki wa mgombea huyo ambao kwa kawaida huwa wengi, jana walijikuta wakiwa idadi sawa kwa mara ya kwanza na watu wanaompinga Trump pamoja na sera zake zinazodaiwa kuwa ni za kibaguzi ,hali iliyozidisha uwezekano wa kuzuka vurugu na kusababisha mkutano kuahirishwa.

Mpinzani wa karibu katika kinyag’anyiro hicho kwenye chama cha Republican,Ted Cruz amesema vurugu hizo zinatokana na matamshi yasiyo na mipaka anayoyatoa mara kwa mara Donald Trump kwa hiyo yeye hashangai kuwa yametimia kwa kutokea fujo kwenye mikutano yake.

0 comments:

Post a Comment