Mama mzazi wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ametoboa siri ya mkaza mwanaye, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kushindwa kuishi Bongo na badala yake kukimbilia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Sandra au Mama D aliyasema hayo katika mahojiano maalum na Ijumaa Wikienda juu ya uhusiano wake na Zari kufuatia tetesi kuwa hawaivi ndipo akaweka mambo sawa.
Mama D alisema kuwa yeye na Zari wapo vizuri lakini kinachomfanya mkwewe huyo kushindwa kuishi naye Bongo ni kutokana na biashara zake kudoda nchini Afrika Kusini.
“Unajua anapokuwa huku (Bongo), biashara zake huwa zinayumba sana, wakati mwingine akipiga simu akiulizia biashara zinakwendaje anaambiwa hali ni mbaya au hazijaingiza chochote hapo ndipo huwa anachanganyikiwa.
“Kwa mfano hivi karibuni alipiga simu akaambiwa hakuna fedha kabisa na biashara haziendi. Kilichofuata ni kujiandaa na kumchukua Tiffah (Latifah Nasibu) kisha akaondoka zake.
“Hicho ndicho kinachomkimbiza Zari kuishi Bongo na si kweli kwamba hapapendi au kuna tatizo lolote,” alisema Mama D.
0 comments:
Post a Comment