Dk.Hamis Kigwangalla Afunguka na Kusema "Poleni CHADEMA Kwa Kumchagua Dkt. Mashinji Kuwa Katibu Mkuu"

Kupitia Account yake ya Facebook Dk Hamisi Kigwangalla anakiri wazi kuwa Dkt. Mashinji ni msomi mzuri na mwanasiasa mzuri ingawa anadai hana uhakika kama alimaliza masomo ya ubingwa.

"Ndg., Dkt. Mashinji is a friend, brother and colleague. Hakuwahi kutuokoa mimi na Dkt. Ulimboka, na hakuwahi kuongoza mgomo, sema alishiriki mgomo ulioongozwa na mimi na Dkt. Ulimboka. Kiukweli, ni mwanasiasa mzuri, msemaji, msomi mzuri (tumesoma naye MBA chuo kimoja), sina hakika kama alimaliza masomo ya Ubingwa maana alinyanyaswa na Supervisor wake, akasusa akaamua kujiiunga masomo ya MBA na sina hakika sana kuhusu 'msimamo usiotetereka'. Maana baada ya vitisho vya 2005, aliyumba sana na tulimtenga na ku-aVoiD kumualika vikao vya CC ya mgomo. Hivyo, kama kigeZo kilikuwa ni hii historia, pole kwa CHADEMA." Ameandika Dk Kigwangalla

0 comments:

Post a Comment