Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Chakula Duniani World Food Programme (WFP), limetunukiwa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2020.

Kamati ya tuzo hiyo nchini Norway imesema kwamba WFP imehusika pakubwa katika juhudi za kuzuia utumiaji wa njaa kama silaha ya vita na mizozo.

Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hiyo mjini Oslo, Berit Reiss Andersen amesema ni vyema dunia kuangaza kuhusu mamilioni ya watu ambao wanakabiliwa na tishio la baa la njaa.

Shirika la Afya Duniani na mwanaharakati wa masuala ya anga Greta Thunberg walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakipigiwa upatu kushinda tuzo hiyo.

Mwaka uliopita tuzo ya amani ya Nobel ilichukuliwa na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ambaye makubaliano yake ya amani na Eritrea yalisitisha uhasama kufuatia vita vyao vya mpakani vya miaka ya 1998-2000.


Haji Manara ni miongoni mwa maafisa habari wa vilabu vya soka vya Tanzania ambao wamedumu katika timu moja kwa muda mrefu, Manara hadi sasa amekaa Simba SC kama afisa habari kwa miaka mitano na miezi mitatu toka pale alipojiunga nayo 2015 mwezi March.

Manara akiongea katika insta Live na Sabrina Golden Hour ameeleza kuwa baada ya kudumu na club hiyo kwa miaka mitano anawaza kutafuta kazi mpya ya kufanya ili apate changamoto mpya.





 Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika, pia ni wa pili kwa urefu Duniani. Mlima huu uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa futi 19,340 (mita 5,895). Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi kuliko mlima tu ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hii mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima. Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko takriban mnamo mwaka 1730. Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru. Mtu wa kwanza wa kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba, 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kijer.:Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani. Kibo ina theluji na barafuto kadhaa ndogo.


Soma Vichwa Habari Vya Magazeti mbali mbali hapa nyumbani Tanzania.












 

Mwigizaji Elizabeth Michael “Lulu” leo amehukumiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia na kusababisha kifo cha Mwigizaji Steven Kanumba.
Baada ya Hukumu hiyo kutolewa Mama Mzazi wa Marehemu Kanumba aliangua kilio na kuongea yafuatayo >>> “Namshukuru Mwenyenzi Mungu, naishukuru Mahakama imetenda haki, naishukuru Serikali yangu awamu ya tano
Kalale salama mwanangu Steven Kanumba na nikitoka hapa nakwenda makaburini naamini nakwenda kumzika akapumzike kwa amani” – Mama Kanumba



















Mechi za  makundi ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi zinafikia ukikongoni huku ikishuhudiwa nchi kadhaa zikifuzu na nyingine maarufu zikikosa nafasi ya kufuzu ambapo nchi kama Marekani na Uholanzi zikikosa sifa ya kucheza fainali hizo.
Wakati Marekani, Chile na Uholanzi zikikosa Fainali za Kombe la Dunia 2018, tayari timu 22 tayari zimejihakikishia kucheza ikiwa ni pamoja na mwenyeji Urusi katika fainali hizo zitakazoshirikisha timu 32.
Zilizofuzu moja kwa moja kutoka katika hatua ya makundi ni;
Bingwa mara tano Brazil, mabingwa watetezi Ujerumani, pamoja na Argentina, Ubelgiji, Colombia, Costa Rica, England, Misri, Ufaransa, Iceland, Iran, Japan, Mexico, Nigeria, Panama, Poland, Ureno, Saudi Arabia, Serbia, Korea Kusini, Uhispania na Uruguay.

Timu nane kutoka Bara la Ulaya zitacheza mechi za mtoano ili kupata timu nne zitakazokamilisha idadi ya timu 14 za Ulaya kufuzu fainali hizo ambapo hadi sasa Bara hilo lina timu 10 ambapo ratiba ya mechi hizo itatolewa October 16 mjini Zurich huku michezo hiyo ikitarajiwa kuchezwa November 9 hadi 11 kwa michezo ya awali na marudiano itakuwa November 12 hadi 14.
Switzerland, Italy, Denmark, Croatia, Ireland Kaskazini, Jamhuri ya Ireland, Sweden na Ugiriki.
Kwa upande wa Amerika ya Kusini, tayari timu nne zimeshafuzu lakini kuna nafasi moja ambapo Peru iliyomaliza nafasi ya tano itacheza mechi ya mtaono dhidi ya New Zealand.

Amerika ya Kaskazini inazo nafasi tatu kujumlisha nafasi ya mtoano ambapo hadi sasa zilizofuzu moja kwa moja ni Mexico, Costa Rica na Panama huku Honduras ikicheza na  Australia kwenye mtoano kupata nafasi ya nne.
Afrika inazo nafasi tano kwenye fainali hizo ambapo hadi sasa ni nchi mbili zilizofuzu ambazo ni Nigeria na Misri huku bado michezo ya makundi  ikiendelea.

NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.
HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.
AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.
VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.
MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali.
AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.
HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba IKIWAPENDEZA wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo.
VILEVILE, nimemua kujiuzulu KITI Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa UCHAGUZI mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua ITIKADI wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania. Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, SOTE kama TAIFA tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu.
Ni maombi yangu kwa MUNGU kuwa Haki itamalaki Tanzania. Upendo, amani na mshikamano wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za Kisiasa, na makabila yote nchini uimarike. Tushindane ki sera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu, na TAIFA lililo imara na nchi yenye ADILI.
#MunguIbarikiTanzania.
Lazaro S. Nyalandu.

Habari zilizotufikia muda huu ni kwamba Mbunge wa Kigoma Mjini ambae pia ni kiongozi wa chama cha ACT WAZALENDO Zitto Kabwe amekamatwa na polisi.

Taarifa zaidi zinasema Zitto amekamatwa akiwa nyumbani kwake Dar es salaam na kupelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe, habari hii imethibitishwa na Afisa Habari wa ACT Wazalendo Abdallah Khamis ambaye ameeleza kuwa sababu za kukamatwa kwake ni hotuba aliyoitoa juzi katika kata ya Kijichi.
Endelea kukaa karibu na habarikwanzabongo.blogspot.com tutakuletea taarifa kamili baadae.

Siku chache zilizopita Mwigizaji wa Tanzania Irene Uwoya amethibitisha kwamba aliefunga nae ndoa ni Msanii wa Bongofleva Dogo Janja, kinachofata sasa ni uthibitisho wa picha. Picha ya kwanza ya harusi yao ndio hiyo hapo juu na imepostiwa na Meneja Babu Tale ambae ameonyesha kufurahia harusi hiyo na kumkaribisha Irene Uwoya kwenye kwenye familia ya TipTop.

Bongo fleva super staa Nedy Music ambaye hivi karibuni amejiunga na lebel ya Ommy Dimopz ya Pozi Kwa Poz amekanusha uvumi kuwa Shilole ni Mpenzi wake...Akihojiwa Clouds FM amesema hana uhisiano wa Kimapenzi na Shilole

Awali Nedy alitajwa akuwa mpenzi wa Shilole baada ya staa huyu kuachana na Nuh Mziwanda



Dj akipagawisha mashabiki


mkongwe banana nae hakua nyuma

jibaba la planet kama kawa


mkatoliki nae